App ya kujisomea mtandaoni ya British School sasa inapatikana Playstore, bonyeza hapa kuisakinisha kwenye simu yako.

Kuhusu Sisi

The British School, ni shule Huria inayotoa mafunzo ya Elimu ya sekondari Huria (Open school education) Wanafunzi wanasoma na kupata cheti cha kidato cha Nne na Sita (Form IV & Form VI). Ambapo wanaanzia ngazi ya QT,( Qualfying test) au Wanaorudia mitihani ya kidato cha Nne na Sita au wale wanaojiunga na kidato cha Sita baada ya kufaulu kinadato cha Nne. Pia Tunafundisha kozi za Computer na Kiingereza kwa watu wote, Kozi ya Ualimu wa chekechea(daycare).... Soma Zaidi

Maono Ya Shule

Kujenga kizazi chenye Mtazamo safi na Ufahamu juu ya mapinduzi ya dunia katika maarifa na ujuzi

(To create a conscious generation with clear mindset on the changes of World knowledge and skills)

Mkakati/Mission

Kutoa maarifa bora na ujuzi kwa wanafunzi wetu kwa kuzingatia mabadiliko ya sasa ya utandawazi duniani.

(To impart Students with best knowledge and skills based on current World globalization)


KARIBU

Principal

Ndugu Mzazi, mwanafunzi na mdau wa elimu uliyetutembelea kwenye wavuti yetu ya THE BRITISH SCHOOL, Shule ya BRITISH ni sehemu salama pa wewe kusoma au kumleta mwanao na ndugu yako ili aweze kutimiza malengo yake ya kielimu, Kwa upande wa masomo ya Sekondari, kozi ya kompyuta na kozi ya Kiingereza.

British school imekua msaada mkubwa sana hapa Nchini kwa Wanafunzi wanaosoma QT, Kidato cha IV, Kidato cha Tano na Sita( kwa mwaka mmoja) na wale wanaorudia mitihani ya QT, Kidato cha IV na VI.

Shule pia imekua ikifaulisha vizuri sana toka kuanzishwa kwake mwaka 2015 hadi sasa.

Mwisho napenda kuwaahidi kuwa British school itaendelea kuhakikisha ufaulu unapanda kila mwaka bila kurudi nyuma, Tutaendelea kuwalea Wanafunzi katika misingi uwajibikaji na kumpenda Mungu..

Ninakukaribisha kwa moyo mkunjufu Ututembelee Shuleni kwetu. maelezo Zaidi.

KARIBUNI NA MUNGU AWABARIKI SANA

CONTACT US

Mwenge ITV Opposite Lutheran church ,
S.L.P 32536, Dar es salaam,
(255) 655 400 420 (255) 755 400 420
info@britishschool.ac.tz