App ya kujisomea mtandaoni ya British School sasa inapatikana Playstore, bonyeza hapa kuisakinisha kwenye simu yako.

Kuhusu Sisi

The British School, ni shule Huria inayotoa mafunzo ya Elimu ya sekondari Huria (Open school education) Wanafunzi wanasoma na kupata cheti cha kidato cha Nne na Sita (Form IV & Form VI). Ambapo wanaanzia ngazi ya QT,( Qualfying test) au Wanaorudia mitihani ya kidato cha Nne na Sita au wale wanaojiunga na kidato cha Sita baada ya kufaulu kinadato cha Nne. Pia Tunafundisha kozi za Computer na Kiingereza kwa watu wote, Kozi ya Ualimu wa chekechea(daycare).... Soma Zaidi

Maono Ya Shule

Kujenga kizazi chenye Mtazamo safi na Ufahamu juu ya mapinduzi ya dunia katika maarifa na ujuzi

(To create a conscious generation with clear mindset on the changes of World knowledge and skills)

Mkakati/Mission

Kutoa maarifa bora na ujuzi kwa wanafunzi wetu kwa kuzingatia mabadiliko ya sasa ya utandawazi duniani.

(To impart Students with best knowledge and skills based on current World globalization)


Principal

KARIBU

Napenda kutumia muda huu kuwashukuru Wazazi,Walezi na Wanafunzi wote, bila kuwasahau Walimu na Wafanyakazi wote wa The British school, kwa moyo wenu wa upendo na uaminifu mliounyesha katika kuijenga shule yetu. Napenda kuwaahidi kuwa, pamoja na kwamba shule imekua ikifanya vizuri tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na matokeo mazuri yaliyoifanya shule kuongoza kwa mwaka wa masomo 2017/2018, nawaahidi kuwa nitaendelea kushirikiana na wafanyakazi wenzangu kwa kuweka bidii kubwa zaidi katika ufundishaji na kuimarisha nidhamu kwa kiwango cha juu Zaidi, ili shule yetu iendelee kuongoza kwa matokeo mazuri kila mwaka.

Asanteni na Mungu azidi kuwalinda na kuwabariki.

“KWA MOYO MKUNJUFU NASEMA, KARIBUNI SANA THE BRITISH SCHOOL”

CONTACT US

Mwenge ITV Opposite Lutheran church ,
S.L.P 32536, Dar es salaam,
(255) 655 400 420 (255) 755 400 420
info@britishschool.ac.tz